Serikali ya Ufaransa imewashauri raia wake walioko nchini Mali kuondoka mara moja “iwezekanavyo” kutokana na hali ya usalama inayoendelea kuzorota kufuatia mashambulizi makubwa ya kigaidi yaliyotokea hivi karibuni.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa, hali ya usalama nchini Mali imeelezwa kuwa “ya hatari kubwa na isiyotabirika”, hasa baada ya mashambulizi yaliyotokea tarehe 25 Aprili katika miji kadhaa ikiwemo Bamako.
Ufaransa imewataka raia wake kutumia safari za ndege za kibiashara zilizopo na pia kupunguza mizunguko isiyo ya lazima huku wakibaki ndani na kufuata maelekezo ya mamlaka za eneo hilo.














