Jeshi la wanamaji la Israel limekamatwa raia 20 wa Uturuki waliokuwa sehemu ya msafara wa meli za misaada wa Global Sumud uliokuwa ukielekea Gaza, baada ya kuzuilia msafara huo katika maji ya kimataifa karibu na kisiwa cha Crete nchini Ugiriki.
Kwa mujibu wa ujumbe wa Uturuki ulioko ndani ya flotilla hiyo, vikosi vya Israel vilizingira meli hizo Jumatano usiku na kuwakamata zaidi ya wanaharakati 170 waliokuwa ndani ya msafara huo.
Msafara huo ulikuwa umebeba misaada ya kibinadamu kwa lengo la kuvunja mzingiro wa muda mrefu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.
CHANZO: TRT Afrika














