Watu watatu wamefariki dunia kwenye meli ya kitalii ya MV Hondius kufuatia mlipuko wa virusi vya hantavirus, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).
WHO imethibitisha kuwa angalau mtu mmoja alipatikana na maambukizi ya hantavirus kupitia vipimo vya maabara, huku watu wengine watano wakishukiwa kuambukizwa.
Mlipuko huo ulitokea wakati meli hiyo ilipokuwa ikisafiri kutoka Argentina kuelekea Cape Verde.
CHANZO: TRT Afrika
















