Ethiopia yawakamata washukiwa 82 wa kundi la kigaidi la Daesh

Mamlaka nchini Ethiopia zimewakamata washukiwa 82 wa kundi la kigaidi la Daesh.

Newstimehub

Newstimehub

15 Julai, 2025

9455804806d543b41e3e61e7d4a836d865df2e5f9824fd4b433863f380bed198

Mamlaka za nchini Ethiopia zimewakamata washukiwa 82 wanaoamini kuwa ni wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh, shirika la kijasusi la nchi hiyo lilisema siku ya Jumanne.

Shirika la Kitaifa la Ujasusi limesema wale waliokamatwa wanashukiwa kupewa mafunzo katika nchi jirani na kisha kuingia katika maeneo mbalimbali nchini Ethiopia.

Wamekamatwa mjini Addis Ababa na katika kanda za Oromia, Amhara, Somali na Harari.

Mamlaka zinasema baadhi ya wale waliokamatwa wanaaminika kuhusika katika vitendo vya uhalifu ikiwemo ukusanyaji wa taarifa za kijasusi, kutoa fedha na kuandaa mipango.

Shirika hilo la kijasusi linasema jamii za maeneo hayo zilisaidia kutoa taarifa zilosaidia kuwakamata na uchunguzi unaendelea kwa sasa.