Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko ya ghafla yaliyokumba mji wa pwani wa Safi nchini Morocco imeongezeka hadi 37, huku operesheni za utafutaji na uokoaji zikiendelea. Mamlaka zinasema tukio hilo ni mojawapo ya majanga mabaya zaidi ya hali ya hewa nchini humo katika zaidi ya muongo mmoja, huku wataalamu wakihusisha ukali wa dhoruba na athari za mabadiliko ya tabianchi.
CHANZO: TRT Afrika














