Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) limetangaza kurejea kwa udhibiti wa mji wa kimkakati wa Uvira, ulioko mpakani na Burundi, baada ya waasi wa M23 kujiondoa. Mji huo, wenye maelfu ya wakazi, ulikuwa umetekwa na waasi tangu mashambulizi ya Desemba, muda mfupi baada ya DRC na Rwanda kusaini makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Rais wa Marekani Donald Trump.
Mnamo Desemba 17, M23 ilitangaza kuondoa vikosi vyake kwa maombi ya Marekani, ingawa baadhi ya wapiganaji wake waliendelea kuwepo. Baadaye, kundi hilo lilisema linapanga kuondoa kikamilifu vikosi vilivyobaki na kuacha mji huo chini ya “udhibiti wa jamii ya kimataifa.”
Kwa mujibu wa msemaji wa FARDC, Mak Hazukay, jeshi la Congo limechukua udhibiti wa mji mzima na linaendelea kupeleka wanajeshi ili kuhakikisha usalama na uthibiti wa maeneo ya jirani.
CHANZO: TRT Afrika














