Ulimwengu

Kiongozi wa upinzani Guinea Bissau awekwa kifungo cha nyumbani

Mahakama ya kijeshi nchini Guinea Bissau siku ya Alhamisi imetoa amri ya kushikwa kwa kiongozi wa upinzani wa nchi hiyo Domingos Simoes Pereira na kuwekwa kifungo cha nyumbani kufuatia tuhuma za kupanga njama ya kupindua serikali.

Newstimehub

Newstimehub

5 Juni, 2026

23b2bb64243d2fc3a23d62b30cb35e8f14df62241e060a98cc20f5bbb0bc2ba6

Mahakama ya kijeshi nchini Guinea Bissau siku ya Alhamisi imetoa amri ya kushikwa kwa kiongozi wa upinzani wa nchi hiyo Domingos Simoes Pereira na kuwekwa kifungo cha nyumbani baada ya kuhojiwa kwa mara nyengine kufuatia tuhuma za kupanga njama ya kupindua serikali, wakili wake amesema.

Pereira, kiongozi wa Chama cha PAIGC, aliwekwa kizuizini wakati jeshi lilipomuondoa madarakani Rais Umaro Sissoco Embalo Novemba 26, 2025.

Aliachiliwa na kuwekwa kifungo cha nyumbani Januari, 2026 lakini anaendelea kushutumiwa kwa kuhusika katika angalau majaribio mawili ya mapinduzi ya 2023 na ya Oktoba 2025.

Ulinzi mkali ulizingira mahakama ambapo Pereira alifika siku ya Alhamisi.

‘Hakujua lolote kuhusu hilo’

Joao Paulo Indeque, mmoja wa mawakili wa Pereira, aliwaambia waandishi wa habari mteja wake amejibu maswali yote ya majaji.

“Domingos Simoes Pereira hakushiriki katika jaribio lolote la kuharibu utaratibu wa kikatiba. Hakujua lolote kuhusu hilo, tuna uhakika wa hilo,” Indeque aliongeza.

Jenerali Horta N’Tam anaongoza serikali ya mpito ya sasa ya Guinea Bissau.