Mamlaka za Madagascar zimemkamata mwanajeshi wa zamani wa Ufaransa, Guy Baret, kwa tuhuma za kushiriki katika njama za kuvuruga usalama wa taifa na kusababisha machafuko nchini humo.
Kwa mujibu wa waendesha mashtaka, Baret anatuhumiwa kupanga hujuma dhidi ya miundombinu muhimu ikiwemo nyaya za umeme, pamoja na kuchochea maafisa wa usalama kufanya uasi dhidi ya serikali.
Mshukiwa huyo amezuiliwa katika gereza lenye ulinzi mkali la Tsiafahy akisubiri hatua zaidi za kisheria.
Mamlaka pia zinasema uchunguzi unaendelea dhidi ya washirika wengine wanaodaiwa kuhusika katika njama hiyo.














