Hifadhi ya wanyamapori karibu na Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imeshuhudia kuzaliwa kwa mapacha adimu wa sokwe wakubwa (gorilla).
Tukio hilo ni la kipekee kwani kuzaliwa kwa mapacha kwa sokwe ni nadra sana duniani. Wataalamu wa uhifadhi wanasema hii ni mara ya pili tukio kama hilo kurekodiwa katika hifadhi hiyo.
Wataalamu wameeleza kuwa watoto hao wako katika hali nzuri, huku juhudi za kuhakikisha usalama wao na mama yao zikiimarishwa. Tukio hili limeongeza matumaini katika juhudi za uhifadhi wa sokwe wakubwa walio hatarini kutoweka.
Chanzo: Africanews














