Mkuu wa zamani wa shirika la ujasusi la Israel Mossad, Tamir Pardo, amekosoa vikali mashambulio ya walowezi wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Pardo amesema matukio aliyoshuhudia katika vijiji vya Palestina vilivyoshambuliwa hivi karibuni yalimkumbusha mateso yaliyowakumba Wayahudi wakati wa Holocaust.
Alisema kuwa kutokana na alichokiona, alihisi “aibu kuwa Myahudi” na kueleza kuwa hali hiyo ni tishio kubwa kwa mustakabali wa taifa la Israel.
Kauli hiyo aliitoa akiwa ameandamana na maafisa wengine wa zamani wa kijeshi waliotembelea maeneo yaliyoathiriwa na mashambulio ya walowezi.
CHANZO: TRT Afrika














