Ulimwengu

Trump Awaambia Waandamanaji wa Iran: “Msaada Unakuja”

“Wazalendo wa Iran, endeleeni kuandamana, chukueni udhibiti wa taasisi zenu!!! Muhifadhi majina ya wauaji na wanyanyasaji. Watalipa gharama kubwa.” — Donald Trump

Newstimehub

Newstimehub

13 Januari, 2026

260

Rais wa Marekani Donald Trump amewataka waandamanaji wa Iran kuendelea kushinikiza mabadiliko kwa kuchukua udhibiti wa taasisi, akiahidi kuwa msaada unakuja na kuwaonya maafisa wa Iran kwamba watalipa gharama kubwa.

Kupitia mtandao wa Truth Social, Trump alisema ameahirisha mikutano yote na wanadiplomasia wa Iran hadi mauaji ya waandamanaji yakome, akitumia kauli mbiu yake maarufu ya Make America Great Again lakini akibadilisha neno Marekani na Iran.

Ikulu ya White House imesema rais ana nia ya kufuata njia ya diplomasia, ingawa msemaji Karoline Leavitt alisisitiza kuwa Trump “haogopi” kutumia nguvu za kijeshi iwapo waandamanaji watashambuliwa.

Kwa upande wake, maafisa wa Iran wameituhumu Marekani na Israel kwa kuunga mkono kile wanachokiita “waasi wenye silaha.” Mashirika ya haki za binadamu yamekadiria kuwa zaidi ya watu 646 wamefariki na zaidi ya 10,000 kukamatwa katika maandamano yaliyosambaa kote nchini tangu kuanza kwa ghasia.

CHANZO: TRT Afrika