Tukio la hatari limeripotiwa nchini Afrika ya kusini ambapo afisa wa polisi alilazimika kushushwa ndani ya mto unaodaiwa kuwa na mamba wengi ili kuokoa mabaki ya mwili wa binadamu.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, tukio hilo lilitokea baada ya kupatikana kwa taarifa kuhusu uwepo wa mabaki ya binadamu ndani ya mto huo, hali iliyohitaji juhudi za haraka za uokoaji licha ya hatari iliyokuwepo.
Afısa huyo alifungwa vifaa maalum vya usalama na kushushwa kwa uangalifu ndani ya maji, huku timu ya uokoaji ikiwa juu tayari kutoa msaada iwapo kungetokea hatari yoyote.
Operesheni hiyo ilifanikiwa kurejesha mabaki hayo, ambayo sasa yamepelekwa kwa uchunguzi zaidi ili kubaini utambulisho wa marehemu na chanzo cha kifo chake.
Tukio hilo limeonyesha hatari zinazokabili maafısa wa usalama wanapotekeleza majukumu yao, hasa katika mazingira magumu na hatarishi kama hayo.
Chanzo:Africanews
















