Rais wa Mali, Assimi Goïta, amesisitiza kuwa hali ya usalama nchini humo iko “chini ya udhibiti” licha ya mashambulizi makali yaliyofanywa na makundi ya kigaidi na waasi wanaoongozwa na Tuareg katika siku za hivi karibuni.
Katika hotuba yake ya kwanza kwa umma baada ya siku tatu za kimya, Goïta alisema vikosi vya usalama vimeimarishwa na operesheni za kusafisha maeneo, utafutaji wa taarifa za kiintelijensia na hatua za kiusalama zinaendelea.
Alikiri kuwa hali ni ya “hatari kubwa” lakini akawataka wananchi kuepuka hofu na migawanyiko, akisisitiza umuhimu wa umoja wa kitaifa.














