Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, ameonyesha wasiwasi kufuatia hatua za jeshi la DRC kuanza kuwanyang’anya silaha wapiganaji wa FDLR walioko nchini humo. Amesema kuwa licha ya makubaliano ya amani ya Washington, bado kinachohitajika ni utekelezaji wa vitendo.
Hatua hiyo imekuja wakati DRC ikiendelea kuhimiza wapiganaji hao kujisalimisha kwa hiari ili kupunguza mapigano katika eneo hilo.
CHANZO: TRT Afrika














