Serikali ya Tanzania imeutaka umma kupuuzia picha mjongeo inayosambaa mitandaoni kuhusu Bunge la Ulaya dhidi ya serikali ya nchi hiyo.
Kulingana na taarifa iliyowekwa kwenye ukurasa wa X wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Bunge la Ulaya haliendeshi mjadala tajwa wa kumuondoa madarakani Rais Samia Suluhu Hassan, kama inavyopotoshwa na baadhi ya wanaharakati mitandaoni.
Tanzania imesisitiza kuwa, video hiyo ni ya Novemba 26, 2025 na hakuna maazimio ya aina hiyo dhidi ya serikali ya nchi hiyo.
“Serikali inaendelea kuwasihi Watanzania kuepukana na usambazaji wa taarifa hizi zenye lengo la kuzua taharuki na kuchochea chuki,” ilisomeka sehemu ya taarifa ya Msemaji Mkuu wa Serikali ya nchi hiyo Gerson Msigwa, kama ilivyowekwa kwenye ukurasa wa X.
Katika picha mjongeo hiyo iliyosambaa mitandaoni, wajumbe wa Bunge la Umoja wa Ulaya, limetaka kufutwa kwa uchaguzi wa Tanzania wa ili ufanyike uchaguzi mwingine.














