Afrika

Tanzania: Watu 130 wakamatwa kwa kuhamasisha vitendo vya kihalifu

Jeshi la Polisi nchini humo, limedai kubaini madai ya mipango mbalimbali ikiwemo kuchoma shule, kuharibu miundombinu ya umeme, kupora mali pamoja na kupanga kushambulia baadhi ya viongozi, wananchi na askari wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Newstimehub

Newstimehub

9 Julai, 2026

f89ceaa2 1418 4f95 8c5d 46b7ece892cf 1783616594658

Jeshi la Polisi nchini Tanzania, linawashikilia watuhumiwa 130 katika mikoa mbalimbali kwa tuhuma za kupanga na kuhamasisha vitendo vya kihalifu vinavyodaiwa kuhatarisha amani na usalama wa taifa.

Kwa mujibu wa taaria iliyotolewa Julai 9, 2026 na msemaji wa jeshi hilo David Misime, watuhumiwa hao wanadaiwa kutumia vikao vya ndani na mitandao ya kijamii kuratibu mipango ya kuvuruga utulivu nchini kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu.

Kulingana na Misime, uchunguzi wa jeshi hilo, umebaini madai ya mipango mbalimbali ikiwemo kuchoma shule, kuharibu miundombinu ya umeme, kupora mali pamoja na kupanga kushambulia baadhi ya viongozi, wananchi na askari wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Amesema hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa baada ya taratibu za uchunguzi kukamilika.