Umoja wa Afrika (AU) umelaani vikali mashambulizi yaliyotokea nchini Mali baada ya mji mkuu Bamako pamoja na maeneo mengine kukumbwa na mashambulizi yaliyotekelezwa na makundi yanayotajwa kuwa ya kigaidi.
Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf alisema mashambulizi hayo yanaweka maisha ya raia katika hatari kubwa na yanapaswa kukomeshwa mara moja.
Youssouf pia alisisitiza kuwa AU itaendelea kusimama pamoja na wananchi wa Mali pamoja na vikosi vya usalama vya nchi hiyo katika jitihada za kurejesha amani na utulivu.
Jeshi la Mali lilisema hali iko chini ya udhibiti na kwamba washambuliaji wamepata hasara kubwa baada ya kukabiliana na mashambulizi hayo.
Mashambulizi mengine pia yaliripotiwa katika miji ya Gao, Kidal kaskazini mwa nchi na Sevare katikati mwa Mali.














