Maelfu ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameanza kurejea makwao wakitokea Burundi kufuatia kuimarika kwa hali ya usalama katika eneo la Uvira.
Kundi la wakimbizi wapatao 470 lilikuwa ni sehemu ya mwisho kurejea, baada ya kukimbia machafuko yaliyotokea miezi minne iliyopita. Wakimbizi hao walikuwa wakihifadhiwa katika kambi ya Busuma iliyoko eneo la Buhumuza.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, hadi kufikia mwezi Machi, takriban wakimbizi 33,000 walikuwa tayari wamerudi nyumbani.
Hatua hiyo imechangiwa na kuondoka kwa waasi wa M23 kutoka maeneo ya Uvira kufuatia shinikizo la kimataifa.
Zoezi la kurejea linaendelea kusimamiwa kwa karibu na mamlaka husika na linatarajiwa kuchukua wiki kadhaa kukamilika.














