Afrika Ajenda

Warsha ya Teknolojia ya Afrika Yawakutanisha Walimu Kutoka Nchi 27 Côte d’Ivoire

Walimu wa robotiki, coding na TEHAMA wapata mafunzo maalum baada ya tamasha la Science Fest Africa.

Newstimehub

Newstimehub

27 Aprili, 2026

706

Warsha kubwa ya teknolojia ya elimu imefanyika nchini Côte d’Ivoire ikiwakutanisha walimu wa robotiki, coding na teknolojia ya habari kutoka nchi 27 za Afrika.

Warsha hiyo iliandaliwa na Türkiye Maarif Foundation kufuatia mafanikio ya tamasha la Science Fest Africa (SFA), lililofanyika Aprili 21. Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea washiriki uwezo katika fikra za kialgorithm, programu za kimwili, utatuzi wa matatizo na matumizi ya teknolojia darasani.

Maafisa waandamizi kutoka Türkiye Maarif Foundation pamoja na Balozi wa Uturuki nchini Côte d’Ivoire walihudhuria hafla hiyo na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza mafunzo baada ya tamasha hilo la kisayansi.

CHANZO: TRT Afrika