Ripoti mpya ya World Meteorological Organization imebainisha kuwa kipindi cha miaka 2015 hadi 2025 ndicho chenye joto kali zaidi kuwahi kurekodiwa duniani. Mwaka 2025 umeorodheshwa kuwa miongoni mwa miaka yenye joto la juu zaidi, ukifikia takriban nyuzi 1.43°C.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, matukio ya hali mbaya ya hewa kama ukame, mafuriko na vimbunga yameongezeka, yakisababisha vifo na hasara kubwa za kiuchumi.
CHANZO: TRT Afrika














