Msanii maarufu wa Nigeria Peter Okoye, anayejulikana kama Mr P, amewajibu wakosoaji waliopinga uamuzi wake wa kubadilisha tarehe ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kutoka Novemba 18 hadi Novemba 30.
Tarehe ya Novemba 18 ilikuwa inashirikiwa na ndugu yake pacha Paul Okoye, jambo lililofanya uamuzi huo kutafsiriwa na wengi kama ishara ya kuvunjika kwa uhusiano wao.
Kupitia mitandao ya kijamii, Mr P alihoji kwa nini watu wanajali sana uamuzi wake binafsi, akisema kuwa si jambo la kuwahusu wengine. Pia alishangaa kwa nini mjadala huo unapata uzito mkubwa kuliko masuala muhimu ya kitaifa.
















