Makao Makuu ya Jeshi la Mali yametangaza kuwa zaidi ya magaidi 100 wameuawa kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa dhidi ya msafara wa makundi yenye silaha magharibi mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi, ndege za kijeshi ziligundua msafara wa pikipiki ukiwa unaelekea kwenye maficho ya wapiganaji magharibi mwa Kolokani, katika mkoa wa Koulikoro kusini mwa Mali.
Jeshi limesema mashambulizi hayo yalifanyika kwa mafanikio, yakiharibu pia vifaa na miundombinu ya kijeshi ya washambuliaji.
Operesheni hiyo ni sehemu ya hatua za kijeshi zilizochukuliwa baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Aprili 25 yaliyoikumba Mali.
















