Magaidi wanaohusishwa na mtandao wa Al-Qaeda wamefanya shambulio kubwa katika mji wa Bagare, kaskazini mwa Burkina Faso, na kusababisha vifo pamoja na uharibifu mkubwa wa mali.
Kwa mujibu wa mashuhuda, washambuliaji waliokuwa na silaha nzito na wakitumia pikipiki walivamia eneo hilo Jumatano mchana, wakifyatua risasi kwa zaidi ya saa moja kabla ya kuchoma moto maduka, magari na pikipiki kadhaa.
Kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo limesema lilichukua udhibiti wa kituo cha kijeshi cha wapiganaji wa Burkina, ingawa halikutoa maelezo zaidi.
CHANZO: TRT Afrika














