Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema vurugu zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 zimemwathiri kwa kiasi kikubwa na kumwekea mzigo mzito wa uongozi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kupokea ripoti ya tume iliyoongozwa na Mohamed Chande Othman, Rais Samia alisema hakutarajia matukio hayo kutokea katika kipindi chake cha uongozi.
Alisisitiza kuwa atabeba jukumu hilo kwa ujasiri na tahadhari, huku akiomba matukio kama hayo yasijirudie tena nchini.
CHANZO: TRT Afrika














