Watu watatu wamefariki dunia papo hapo kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea jijini Dodoma nchini Tanzania, majira ya alfajiri.
Kwa mujibu wa taarifa, ajali hiyo ilitokea karibu saa 12 asubuhi na kusababisha moto mkubwa kuzuka mara baada ya tukio hilo, hali iliyoongeza ugumu katika juhudi za awali za uokoaji.
Mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wamesema hali ilikuwa ya kutisha huku taharuki ikitanda kutokana na moto uliokuwa ukiwaka kwa kasi.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limethibitisha vifo vya watu watatu na kusema miili ya marehemu ilitolewa baada ya operesheni ya kuzima moto kukamilika.














