Miezi miwili baada ya Marekan kuahidi kuimarisha juhudi za kupambana na ugaidi nchini Nigeria kupitia msaada wa kijasusi, mafunzo, na ushirikiano wa kimkakati, hali imechukua mwelekeo tofauti kufuatia ongezeko la matukio ya ukosefu wa usalama.
Taarifa mpya zinaonyesha kuwa Washington imeagiza wafanyakazi wasio wa muhimu wa ubalozi wake pamoja na familia zao kuondoka katika mji mkuu Abuja, ikitaja kuongezeka kwa vitisho vya kiusalama kama sababu kuu ya uamuzi huo. Hatua hiyo imezua wasiwasi kuhusu hali halisi ya usalama nchini humo na ufanisi wa juhudi za kimataifa katika kukabiliana na ugaidi.
Chanzo: TRT Afrika














