Usalama

Uganda ipo tayari kuisaidia Israel vitani, asema Jenerali Muhoozi

Licha ya kutaka kukomeshwa kwa vita hivyo, Jenerali Muhoozi alisema kuwa Uganda itakuwa tayari kuisaidia Israel katika vita dhidi ya Iran.

Newstimehub

Newstimehub

26 Mechi, 2026

e7e4564ee627881e826e00f8d6874f845007bb3bfd6292547b1af3f85ef452bb

Mkuu wa Majeshi wa Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba amesema kuwa nchi yake ipo tayari kuisaidia Israel katika vita vya Mashariki ya Kati, iwapo taifa hilo litashindwa.

“Tunataka kuona vita vya Mashariki ya Kati vikiisha mara moja kwani dunia imeshachoka sasa. Hata hivyo, hatutosita kuingia vitani na kuisaidia Israel iwapo taifa hilo litaonekana kushindwa mapambano,” aliandika Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni, kupitia mtandao wa X, siku ya Jumatano.

Kauli ya Jenerali Muhoozi inakuja huku vita vya Marekani-Israel dhidi ya Iran vikiendelea kupamba moto katika eneo la Mashariki ya Kati.

Chanzo: Africanews