Hali ya wasiwasi imeongezeka katika Bamako baada ya makundi ya wanamgambo wa Kiislamu kukaza mzingiro na kuzuia njia muhimu za usafiri kuelekea na kutoka mji huo,
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wakaazi, barabara kuu zimefungwa au kudhibitiwa na wapiganaji, hali inayosababisha watu wengi kushindwa kusafıri au kurejea nyumbani. Wengi wamekuwa wakijiuliza kwa hofu: “Tutarudi vipi nyumbani?” kutokana na hali hiyo.
Mzingiro huo umeathiri kwa kiasi kikubwa usambazaji wa bidhaa muhimu kama chakula, mafuta na dawa, huku bei zikiongezeka kwa kasi ndani ya mji,serikali ya Mali imeeleza kuwa inaendelea kuchukua hatua za kijeshi ili kurejesha udhibiti wa maeneo yaliyotekwa, lakini hali bado ni tete.
Mashirika ya kibinadamu yameonya kuwa ikiwa hali itaendelea, inaweza kusababisha mgogoro mkubwa wa kibinadamu, hasa kwa wananchi wanaotegemea usafıri wa kila siku kwa shughuli zao.
Chanzo:BBC News














